KARIBU KWENYE TOVUTI YA SHULE YA SEKONDARI KISHUMUNDU
Shule ya Sekondari Kishumundu ili anzishwa mwaka 1985 ni Shule inayomilikiwa na Kanisa Katoliki jimbo kuu la Moshi, Shule ipo Uru Kishumundu ni umbali wa kilomita 9 kutoka Moshi mjini.
Shule ya Sekondari Kishumundu inafundisha michepuo ya Biashara na sayansi pamoja na sanaa.
Masomo ya sayansi yanayofundishwa shuleni ni Baiologia, Fizikia, Kemia, Hisabati pamoja na masomo ya sanaa kama. Historia, Kiswahili, Jiografia, uraia na Kiingereza na masomo ya Biashara na utunzaji wa Mahesabu, pia Shule inafundisha masomo ya Sayansi na Teknolojia kama kompyuta na masomo ya Vitendo.
KUFUNDISHA KWA MAFANIKIO
Katika miaka ya hivi Karibuni Shule yetu ilifikia nafasi nzuri sana katika
mitihani ya mwisho ya kitaifa ya CSEE ya wanafunzi wa kidato cha IV.
Kwa kawaida tuko ndani ya asilimia 15-20 inayoongoza ya Shule zote
za Tanzania, tazama grafu hapa chini. Ukipenda tafadhali jiangalie
mwenyewe matokeo yetu ya miaka iliyopita mtandaoni.
2022: https://matokeo.necta.go.tz/csee2022/results/s0492.htm
2021: https://onlinesys.necta.go.tz/results/2021/csee/results/s0492.htm
2020: https://onlinesys.necta.go.tz/results/2020/csee/results/s0492.htm
2019: https://onlinesys.necta.go.tz/results/2019/csee/results/s0492.htm
Gari jipya la Shule ya Sekondari Kishumundu kutoka kwa wadhamini wanaotokea shule ya Ujerumani inayoitwa (Helfen macht Schule).
Mnara wa Internet ukiwa kwenye matengenezo kwa ajili ya huduma ya Internet katika Shule ya Sekondari Kishumundu.